TUNA NIA YA KUBORESHA MIUNDO MSINGI ZAIDI MJINI: GAVANA MANDAGO

TUNA NIA YA KUBORESHA MIUNDO MSINGI ZAIDI MJINI: GAVANA MANDAGO

Serikali gatuzi ya Uasin Gishu inaweka mikakati kuona kuwa mji wa Eldoret unaimarishwa kwa kiwango cha kuwa jiji.

Gavana Jackson Mandago amesema kuwa serikali yake imeweka misingi dhabiti ili kufanikisha ruwaza hii ambayo itaifanya Eldoret kuwa jiji la nne nchini Kenya.

Akiongea katika mkutano na maafisa kutoka kitengo cha “Sustainable Urban Economic Development (SUED) program” afisini mwake, Gavana Mandago alisema ruwaza hii itafaulu kupitia ushirikiano na washirika.

Serikali yangu imeweka mikakati kufanikisha Eldoret kuwa mji. Yamkini tunatazamia kufanikisha ruwaza hii kufikia mwaka ujao,” kasema Mandago.

Mandago aliendelea, “Tuko na nia ya kuacha mji huu na miundo misingi mizuri zitakazovutia uwekezaji.”

Tumefaulu kupanua na kuboresha mazingira ya biashara, kuwapa wananchi nafasi ya kutosha kupitia kuboresha barabara nyuma mwa mji,” akaongeza Gavana.

Serikali gatuzi inapanua miundo msingi ikiwemo njia katikati mwa mji wa Eldoret, na miji zinazostawi kama vile Turbo, Burnt Forest, Moi’s Bridge na kuboresha barabara ndogo katika vitongoji duni kama Langas, Kamukunji, Munyaka, Huruma na nyinginezo.

Katika kuweka Eldoret tayari kufikia kiwango cha jiji, serikali ya kaunti inajenga mradi wa maji katika bwawa la Kipkaren Airport, ikipangia kuwanywesha maji wakaaji wa Kapseret, Langas, Kipkenyo na mitaa mingine.

Hizi ni baadhi ya miradi zinazotekelezwa na serikali ya kaunti ikishirikiana na mashirika tofauti zikiwemo Benki Kuu ya Dunia, shirika la UKAid na zinginezo.

Waliohudhuria mkutano huo ni Waziri wa Ardhi na Ustawi wa Mji, (Mhandisi) Nelson Maritim, mwenyekiti wa Bodi ya Manispaa ya Eldoret, Julius Kitur, Afisa Mkuu katika idara ya ardhi, Kenneth Mbeka na meneja wa mji wa Eldoret, Tito Koiyet.

Bi Monica Motshengwe aliongoza uwakilishi wa SUED, ambayo ni mpango chini ya shirika la UKAid, la kuisaidia manispaa ya Kenya kustawi kimiundo msingi.

F
F
Twitter
UGC_TheChampion on Twitter
Latest Tweet:
0 people follow UGC_TheChampion

F