TULIPE USHURU HUDUMA ZIIMARIKE, MANDAGO AWAAMBIA WANABIASHARA

TULIPE USHURU HUDUMA ZIIMARIKE, MANDAGO AWAAMBIA WANABIASHARA

Wanabiashara na wakaazi wa kaunti ya Uasin Gishu wamehimizwa kulipa kodi kwa wakati ili kufanikisha oparesheni za jimbo na kuboresha huduma.

Kodi inasaidia serikali kupata fedha za kufanikisha oparesheni kadhaa kama kukarabati barabara, kusambaza maji na huduma nyinginezo.

Akiongea katika hafla ya uzinduzi wa duka kuu la Khetia Garments, Gavana Jackson Mandago amewarai wafanyi biashara kulipa kodi.

“Tunawaomba wanabiashara kuchukua leseni na kuipa serikali fedha ambazo zitafanikisha uboreshaji wa mazingira ya kufanya biashara zaidi,” kasema Mandago.

Gavana alisema haya huku serikali yake ikiendelea kukarabati barabara za mjini na za nyuma (backstreets) ili kupanua nafasi za biashara. Vibanda zinaendelea kujengwa mjini ili kuwekeza nafasi zaidi za biashara.

Kaunti ya Uasin Gishu iliorodheshwa na Benki ya Dunia kwa urahisi wa kuanzisha na kufanya biashara na kama eneo bora la uekezaji.

Mashirika kadhaa kama Safaricom, Toyota, Nova Pioneer Schools, benki na kampuni zingine zimewekeza mabilioni ya fedha katika biashara mjini Eldoret.

Naibu mwenyeketi wa chama cha ushirika wa wanabiashara (KNCCI) tawi la Uasin Gishu Bw. Willy Kenei amesema: “Mazingira ya biashara inaendelea kuwa bora mjini na nawahimiza wenzangu tulipe kodi ili tuwe na mazingira bora na biashara zetu zipanuke.”

Na Mandago alitoa hakikisho ya utumizi wa fedha.

“Nawahakikishia kuwa pesa hizi za kodi na zote za umma zinatumika ipasavyo na serikali yangu inawajibika kwa matumizi ya fedha zote tunazozipokea,” alisema Mandago huku akisisitiza kuwa hajawahi kosa kufika kwenye kamati ya fedha ya Seneti akiitwa kujibu maswali ya utumizi wa fedha za Kaunti.

Waziri wa Fedha, CPA Julius Ruto amesema: “Serikali ya kaunti inahitaji fedha ili kukarabati njia, kuwapa maji na kuweka mazingira bora ya biashara, hivyo tuendelee kulipa kodi.

“Tumefanikisha ukataji wa leseni kwa kupitia mtandao, ili kupunguza msongamano na kurahisisha huduma hii.”

“Unawezapata leseni yako kupitia mtandao bila kufika kwa ofisi kuu,” waziri wa Biashara na Mawasiliano, Dkt Emily Kogos amesema, mwenzake wa Ushirika, Esther Mutai akihimiza vyama vya ushirika.

Meneja Mkurugenzi wa Khetia Garments, Krish Khetia amesema. “Gavana Mandago, nakukushukuru na serikali yako kwa kufanikisha uboreshaji wa mazingira ya kufanya biashara. Njia kwa mfano ni nzuri na imetuwezesha kusafirisha mauzo yetu hadi kwa maeneo tofauti.”

Mkurugenzi wa ukusanyaji wa ushuru, CPA Jonah Lamai alikuwa miongoni mwa viongozi waliohudhuria hafla hiyo.

Khetia Garments ni duka kuu linalohudumia kaunti nane za kaskazini mashariki na Magharibi mwa taifa la Kenya.

F
F
Twitter
UGC_TheChampion on Twitter
Latest Tweet: RT @GvnMandago: Was privileged to host 4 Ambassadors from Nordic countries, the envoys from @SwedeninKE, @NorwayInKenya, @FinnishEmbNBO & @…
10,569 people follow UGC_TheChampion
Twitter Pic chewen_v Twitter Pic Monniequ Twitter Pic jogori20 Twitter Pic Sutah_Is Twitter Pic bomerkip Twitter Pic ArapKirw Twitter Pic jeneby_a Twitter Pic kiturphy
F