IMEBIDI WAZEE WAWE MITA 5 MBALI NA WAJUKUU

IMEBIDI WAZEE WAWE MITA 5 MBALI NA WAJUKUU

Gavana Jackson Mandago amewataka wazee kujiepusha na shughuli za kimaisha zinazoweza kuwafanya kuambukizwa na virusi vya korona.

Gavana amesema haya huku idadi kubwa ya vifo vya hivi majuzi vikiwa vya wazee ambao wamezidi umri wa 50, chanzo cha maafa ikiwa homa ya korona. Idadi ya maambukizi inazidi kupanda.

Yaamkini kwa sasa, wazee wanaathirika sana na maradhi haya kwani kinga yao ya mwili inasemekana kuwa chini hivyo basi kuzidiwa na makali ya ugonjwa huu wa Korona.

¬†Maradhi haya yanasambaa kwa kasi na makali yake yako juu sana, tafadhali nawaomba wazazi mjiepushe na kutangamana na watoto na vijana ambao miili yao yana uwezo wa kupambana na ugonjwa huu hata wakiambukizwa,” alisema Mandago.

Kinga ya mwili ya vijana ina uwezo imara wa kupigana na maradhi haya, wanaeza kuwa wameambukizwa lakini hawaonyeshi dalili zozote na hivyo basi wanaweza eneza maradhi haya pasipo kujua,” aliongeza Gavana.

Aliendelea: “Sote tunawapenda wajukuu hawa lakini ni bore wazee kuwasalimu na kuwabariki wakiwa mbali kwa sababu madhara yanawezakuwa mabaya. Wasalimie wakiwa mita karibu tano mbali ili sote tuwe salama, yamkini hadi korona ituondokee.”

Gavana Mandago pia amewaomba wakenya kwa jumla kutolegeza kamba dhidi ya vita vya kupigana na ugonjwa huu wa Korona haswa kuvalia maski ipasavyo, kunawa mikono kwa maji ya sabuni kila wakati au kutumia vyeuzi na kuepuka umati.

Naibu wake, Daniel Chemno, alisema ni bora kuzuia kuliko kuponya, akiongeza kuwa itabidi shughuli mpya za kimaisha zitazingatiwa hadi waktai ambapo korona itaondoka. Itabidi binadamu aoshe mikono, aacha salamu za mikono na kuvaa barakoa hadi homa hii iondoke.

Serikali ya kaunti ya Uasin Gishu linakabiliana na korona ipasavyo kwa kukagua magari ya uchukuzi, mikahawa na sehemu za burudani ili kuimarisha kinga.

F
F
Twitter
UGC_TheChampion on Twitter
Latest Tweet: TRANSFORMING THE COOPERATIVE MOVEMENT THROUGH THE COUNTY ENTERPRISE FUNDS:- Watch it Here https://t.co/HZjhIzZBrj via @YouTube
10,926 people follow UGC_TheChampion
Twitter Pic DOUGLASM Twitter Pic DanielK9 Twitter Pic sanja799 Twitter Pic c_a_chal Twitter Pic Oyomba3 Twitter Pic netgig Twitter Pic Felix678 Twitter Pic dubaiage
F