Gavana awataka wenyeji kujiepusha na hulka ya kusubiri dakika ya mwisho kujisajili kuwa wapiga kura

Gavana awataka wenyeji kujiepusha na hulka ya kusubiri dakika ya mwisho kujisajili kuwa wapiga kura

0L4A0346

Gavana wa Uasin Gishu Jackson Mandago amesema amefanya mkutano na maafisa wasimamizi wa Hospital ya mafunzo na Rufaa ya Moi mjini Eldoret kwa lengo la kupunguza gharama ya huduma za matibabu kwa wananchi.

Mandago aidha alisema mkutano huo ulijadili namna ya kuwasaidia wale ambao vitambulisho vyao vinazuiliwa kutokana na kushindwa kulipa ada za matibabu ili warejeshewe na kuwawezesha kujisajili kuwa wapiga kura.

Aidha aliwataka wenyeji kujiepusha na hulka ya kusubiri hadi dakika mwisho ili kujisajili kuwa wapiga kura.

Gavana aidha alifichua kuwa serikali yake imetenga shilingi milioni 20 kujenga kituo cha akina mama kujifungua katika Hospitali ya Kapteldon, kaunti ndogo ya Kapseret.

Alisema hayo wakati wa hafla ya mazishi katika eneo la Kapmoson.

F
F
Twitter
UGC_TheChampion on Twitter
Latest Tweet: @UGC_TheChampion in partnership with Norrkoping municipality from Sweden lays out measures aimed at heightening the… https://t.co/LISfK6mU2U
7,409 people follow UGC_TheChampion
Twitter Pic Beatrice Twitter Pic CBikramh Twitter Pic NewtonCh Twitter Pic ocsgroup Twitter Pic ncheruiy Twitter Pic KelvinKi Twitter Pic SusanRot Twitter Pic nyalosi
F